Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida ametangaza vikwazo zaidi dhidi ya Urusi. Vikwazo hivyo amevitangaza akihitimisha ziara yake ya Kusini-mashariki mwa Asia na Ulaya.
–
Vikwazo hivyo ni pamoja na kufungia mali za takriban Warusi 140 na baadhi ya benki za Urusi. Vyombo 70 vya kijeshi vitaongezwa kwenye marufuku ya kuuzwa nje ya Urusi na vifaa vya kompyuta kutoka nchini humo.
–
Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida, “Japani na mataifa mengine ya G7 haitavumilia vitisho vya Urusi, na Japan inasimama na Ukraine,”. Vikwazo hivi vinakuja baada ya Urusi kutangaza marufuku ya viongozi 63 kutoka Japan kuingia Urusi akiwemo Fumio Kishida.