Mkazi wa kijiji cha Lugarawa wilayani Ludewa Mkoani Njombe Ombeni Ngwa’vi (25) amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela kwa kosa la kuvunja nyumba na miaka miwili kwa kosa la kuiba debe moja la maharage ambapo vifungo hivyo vitaenda kwa kufuatana na si sambamba.
–
Akisomewa shitaka hilo katika mahakama ya mwanzo Lugarawa na Mwendesha mashtaka Asifiwe Asajile mbele ya Hakimu Timoth Mwakisambwe imedaiwa kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo mnamo Mei 12 mwaka huu majira ya mchana ambapo alivunja nyumba ya Evaristo Mgimba kisha kuiba debe moja la maharage yenye thamani ya shilingi 30,000.
–
Mtuhumiwa huyo amekiri kutenda kosa hilo ikiwa ni kinyume na kifungu cha sheria namba 294(1)(a), 258(1) na 265 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 marejeo ya 2019.