Shabiki wa klabu ya Nottingham Forest Robert Biggs (30) amehukumiwa kifungo cha miezi 6 jela kwa kumshambulia kwa kumpiga kichwa nahodha wa klabu ya Sheffield United, Billy Sharp mwishoni mwa mchezo wa nusu fainali ya mchujo wa kupanda daraja.
ADVERTISEMENT
–
ADVERTISEMENT
Nottingham Forest ilishinda kwa changamoto ya mikwaju ya penalti 3-2 dhidi ya Sheffield United na kutinga fainali ambapo itachuana na Huddersfield.