ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Sunday, October 1, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result

JOGOO AGOMA KUUZWA

Shabani Rapwi by Shabani Rapwi
May 24, 2022
in HABARI
0
JOGOO AGOMA KUUZWA
0
SHARES
500
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Wenyeji katika kijiji kimoja cha Luanda Kaunti ya Vihiga nchini Kenya waliachwa na mshangao mkubwa na kuchanganyikiwa baada ya jogoo anayedaiwa kuibwa katika Kaunti nyingine kukataa kuuzwa licha ya bei yake nafuu.

RelatedPosts

CHAGUZI KUFANYIKA MTANDAONI SIKU ZIJAZO

CHAGUZI KUFANYIKA MTANDAONI SIKU ZIJAZO

Sep 29, 2023

TSO WAZINDUA GALA DINNER

Sep 29, 2023

CHANJO YA MBWA NI MUHIMU

Sep 29, 2023
Load More

 

–

Mwizi aliyekuwa amemleta jogoo wa kuiba katika soko la Luanda alijikuta matatizoni baada ya kutaka kumuuza jogoo huyo na alichanganyikiwa kama walivyochanganyikiwa wengine, baada ya kugundua kuwa, Jogoo huyo kutoka Kaunti ya Siaya, alimkatalia mwizi (kwa jina William) kila mara alipotaka kumuuza.

 

–

Tukio hilo lilitokea na kujirudia mara 4 hadi watu waliokuwa sokoni walipoanza kushuku na kuamua kumkabili mtu huyo na kumhoji kumhusu jogoo huyo ambaye bei yake ilikuwa ndogo tofauti na ukubwa wa jogoo.

 

–

Wafanyabiashara katika soko hilo, walimhoji William na kutaka kufahamu ni kwa nini jogoo huyo alikuwa akionyesha tabia isiyokuwa ya kawaida na alishindwa kuwajibu kwa ufasaha. Baada ya muda wakimhoji, kumbe taarifa ilikuwa imemfikia mwenye jogoo ambaye alifika na hatimaye kumtambua kuku wake aliyekuwa ametoweka kwa kuwa soko hilo lipo mpakani, inadaiwa mwenye kuku huyo alikuwa amefika katika soko hilo na alikuwa akimsaka kuku huyo.

 

–

Katika hali ya kushangaza sana, mtu huyo alisema amefanya urafiki mkubwa na mifugo wake, na kwamba ni vigumu mtu yeyote kumwibia na aliondoka na kuku wake huku mhusika wa wizi akiponea kichapo kwa kupigwa na umma. Hata hivyo, ilidaiwa mwenye jogoo huyo ni mganga ambaye nguvu zake na dawa zilichangia kuku huyu kukataa kununuliwa kwani sio hali ya kawaida.

Related

Shabani Rapwi

Shabani Rapwi

Related Posts

CHAGUZI KUFANYIKA MTANDAONI SIKU ZIJAZO
HABARI

CHAGUZI KUFANYIKA MTANDAONI SIKU ZIJAZO

by SUZO SHUKRANI
Sep 29, 2023
TSO WAZINDUA GALA DINNER
HABARI

TSO WAZINDUA GALA DINNER

by SUZO SHUKRANI
Sep 29, 2023
CHANJO YA MBWA NI MUHIMU
AFYA

CHANJO YA MBWA NI MUHIMU

by SUZO SHUKRANI
Sep 29, 2023
52 WAFARIKI KWENYE MAADHIMISHO YA MAULID NCHINI PAKISTAN
HABARI

52 WAFARIKI KWENYE MAADHIMISHO YA MAULID NCHINI PAKISTAN

by SUZO SHUKRANI
Sep 29, 2023
SEKTA YA MADINI YAJA NA MBT KAMA FURSA KWA VIJANA
HABARI

SEKTA YA MADINI YAJA NA MBT KAMA FURSA KWA VIJANA

by SUZO SHUKRANI
Sep 29, 2023
TUNZAA YATANGAZA USHIRIKIANO MKUBWA NA KAMPUNI YA VODACOM KUPITIA M-PESA 
HABARI

TUNZAA YATANGAZA USHIRIKIANO MKUBWA NA KAMPUNI YA VODACOM KUPITIA M-PESA 

by I am Krantz
Sep 29, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

May 2022
M T W T F S S
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031  
« Apr   Jun »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In