ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Friday, March 24, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

KAMPENI YA UCHUNGUZI WA KIFUA KIKUU YAPOKELEWA KWA SHANGWE NA WAKAZI WA KATA YA RUVUMA NA BOMBAMBILI

Ally Hamis Zingizi by Ally Hamis Zingizi
May 14, 2022
in HABARI
0
KAMPENI YA UCHUNGUZI WA KIFUA KIKUU YAPOKELEWA KWA SHANGWE NA WAKAZI WA KATA YA RUVUMA NA BOMBAMBILI

OLYMPUS DIGITAL CAMERA

0
SHARES
128
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT

Baadhi ya wakazi wa kata ya Ruvuma katika  Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wakisubiri kupata huduma ya uchunguzi wa ugonjwa wa kifua kikuu inayotolewa bure na wizara ya Afya kwa kushirikiana na wadau wa Maendeleo Shirika la MDH na Amref Health Africa.

Wahudumu wa Afya ngazi ya jamii(CHW)wakiwasikiliza baadhi ya wananchi waliofika kupata huduma ya uchunguzi wa kifua kikuu  wakati wa kampeni ya uchunguzi wa ugonjwa huo inayotolewa bure na wizara ya Afya kupitia kitengo cha kifua kikuu na ukoma Hospitali ya mkoa wa Ruvuma kwa kushirikiana na Shirika lisilo la Kiserikali la MDH-Amref Health Africa.

Muhudumu wa Afya ngazi ya jamii9CHW) kata ya Ruvuma katika Manispaa ya Songea Aziza Kivina kulia,akimsikiliza mkazi wa mtaa wa Mibulani Hadija Mohamed aliyefika kupata huduma ya uchunguzi wa ugonjwa wa kifua kikuu wakati wa kampeni ya kupambana na ugonjwa wa TB inayolenga kuibua na kuwaanzishia dawa wale watakaobainika kuwa na  ugonjwa huo.

Wahudumu wa ngazi ya jamii(CHW) kata ya Bombambili wakiendelea na majukumu ya kuhudumia wananchi wakati wa kampeni hiyo.

Baadhi ya wakazi wa Mtaa wa Melikebu kata ya Bombambili Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wakisubiri kufanyiwa uchunguzi wa vimelea vya ugonjwa wa kifua kikuu kutoka kwa wataalam wa afya.

RelatedPosts

MESUT ÖZIL ATANGAZA KUSTAAFU SOKA

MESUT ÖZIL ATANGAZA KUSTAAFU SOKA

Mar 23, 2023

WABUNGE WAONYA KUWEKEA VIKWAZO SHERIA YA MAPENZI YA JINSIA MOJA

Mar 23, 2023

UWANJA WA NDEGE CHATO KUBORESHWA

Mar 23, 2023
Load More

Na Muhidin Amri,
Songea

KAMATI ya usimamizi wa Huduma za Afya ya mkoa wa Ruvuma kwa kushirikiana na  shirika lisilokuwa la Kiserikali la MDH-Amref Health Africa, imeanza Kampeni ya uchunguzi wa ugonjwa wa kifua kikuu kwa wananchi wanaoishi katika mazingira duni na hatarishi.

Maeneo hayo ni kata ya Ruvuma na Bombambili  katika Manispaa ya Songea,ambayo yanatajwa kuwa na idadi kubwa ya wagonjwa wa kifua kikuu katika wilaya ya Songea mkoani Ruvuma.

Akizungumza jana,Mratibu wa kifua kikuu na ukoma mkoa wa Ruvuma Dkt Xavier Mbawala alisema,kampeni hiyo  imehusisha kata  hizo kutokana na wakazi wake wengi kuishi kwenye makazi duni ambayo ni hatarishi na rahisi kupata ugonjwa huo.

Alisema,moja ya  makundi hatarishi yaliyoko katika hatari ya kupata maambukizi  ya kifua kikuu ni umaskini katika jamii ikiwamo kuishi  chumba kimoja watu wengi,nyumba zisizokuwa na mwanga na hewa ya kutosha.

Alisema, ndiyo maana Serikali ya mkoa  kupitia wataalam wa kitengo cha kifua kikuu na wadau wa mandeleo Shirika la MDH na Amref Afrika imedhamiria kutokomeza kabisa ugonjwa huo ifikapo mwaka 2035.

Kwa mujibu wa Dkt Mbawala ni kwamba,katika kuhakikisha mpango huo unafanikiwa wameanza  kwenda kila wilaya kutoa elimu na kufanya uchunguzi wa ugonjwa huo ili jamii iweze kufahamu na kuchukua hatua  ya haraka ikiwamo kuwahi Hospitali kupata matibabu.

Dkt Mbawala alisema, kampeni  hiyo itafanyika katika wilaya zote za mkoa huo na matumaini kuwa italeta tija kubwa na itasaidia  kuokoa maisha ya watu ambao wameambukizwa ugonjwa huo lakini wameshindwa kwenda katika vituo vya kutolea huduma za matibabu kutokana na sababu mbalimbali.

Dkt Mbawala alieleza kuwa,ugonjwa wa kifua kikuu unatibika  na muhimu kwa mtu aliyepata ugonjwa huo kuwahi haraka ili kuepuka vifo na kuambukiza wengine.

ADVERTISEMENT

“Serikali yetu ya mkoa wa Ruvuma inashirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo ikiwamo MDH- Amref  Health Africa katika kuboresha huduma za afya  ili kwa pamoja tuweze kutokomeza ugonjwa wa kifua kikuu ifikapo mwaka 2035”alisema.

Kwa upande wake Mratibu wa kifua kikuu na ukoma Manispaa ya Songea Dkt Emanuel Kiwale alisema, hali ya maambukizi ya kifua kikuu katika manispaa ya Songea ni makubwa ambapo amezitaja kata zinazoongoza kuwa na wagonjwa wengi wa kifua kikuu ni Ruvuma na Bombambili.

Dkt Kiwale alisema, hali hiyo inachangiwa sana na umaskini kwa wakazi wake ambapo wanalazimika kuishi  watu wengi  katika chumba  au nyumba moja isiyokuwa na mwanga au hewa ya kutosha.

ADVERTISEMENT

Baadhi ya wakazi wa kata ya Ruvuma,wameipongeza Serikali kupeleka huduma ya uchunguzi katika maeneo yao kwani itasaidia sana kuokoa maisha ya watu wengi hasa wazee ambao hawawezi kufika kwenye vituo vya kutolea huduma.

Hadija Ismaila alisema,kuna watu wanasumbuliwa na ugonjwa  huo kwa muda mrefu lakini wameshindwa kwenda kupata matibabu  kwenye  vituo na Hospitali kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo nauli ya kutoka nyumbani hadi Hospitali.

Alisema,badala yake wanaendelea kuteseka na hata wapo waliopoteza maisha na kuiomba Serikali na wadau wa afya kuhakikisha wanasogeza huduma zake karibu na wananchi badala ya  huduma hizo kupatikana makao makuu ya kata,wilaya na mkoa.

Ibrahim Salum alisema,huduma hiyo ni nzuri kwani inatoa majawabu ya shida za wananchi  wenye maradhi ambao wana tabia ya kumeza dawa bila kupata ushauri wa Madaktari.

Amewapongeza watoa huduma  kwa kazi wanaofanya ya uchunguzi wa ugonjwa wa kifua kikuu kwa wananchi,na kuwataka kuendelea  kuwasaidia watu ambao wanakabiliwa na changamoto nyingi za kimaisha ikiwamo maradhi ya mara kwa mara.
MWISHO.

OLYMPUS DIGITAL CAMERAOLYMPUS DIGITAL CAMERAOLYMPUS DIGITAL CAMERAOLYMPUS DIGITAL CAMERAOLYMPUS DIGITAL CAMERA

Related

ADVERTISEMENT
Ally Hamis Zingizi

Ally Hamis Zingizi

Related Posts

WABUNGE WAONYA KUWEKEA VIKWAZO SHERIA YA MAPENZI YA JINSIA MOJA
HABARI

WABUNGE WAONYA KUWEKEA VIKWAZO SHERIA YA MAPENZI YA JINSIA MOJA

by ALFRED MTEWELE
Mar 23, 2023
UWANJA WA NDEGE CHATO KUBORESHWA
HABARI

UWANJA WA NDEGE CHATO KUBORESHWA

by ALFRED MTEWELE
Mar 23, 2023
ASHTAKIWA MAHAKAMANI KUWAINGILIA MBUZI KIMWILI
HABARI

ASHTAKIWA MAHAKAMANI KUWAINGILIA MBUZI KIMWILI

by ALFRED MTEWELE
Mar 23, 2023
NMB yatoa msaada wa milioni 39 kuimarisha sekta ya afya na elimu Kanda ya Kati
HABARI

NMB yatoa msaada wa milioni 39 kuimarisha sekta ya afya na elimu Kanda ya Kati

by I am Krantz
Mar 23, 2023
Yaliojili Kwenye Kurasa za Magazeti ya Leo Jumatatu Februari 6,2023
HABARI

Yaliojili Kwenye Kurasa za Magazeti ya Leo Alhamisi Machi 23,2023

by ALFRED MTEWELE
Mar 23, 2023
YANGA PRINCESS, SIMBA QUEENS HAKUNA MBABE
HABARI

YANGA PRINCESS, SIMBA QUEENS HAKUNA MBABE

by Shabani Rapwi
Mar 22, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
May 2022
M T W T F S S
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031  
« Apr   Jun »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In