Shirikisho la Soka Afrika limefikia makubaliano ya kuitoa timu ya taifa Kenya kushiriki kwenye michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) 2023 licha ya awali kujumuishwa kwenye makundi huku kesi yao ikiendelea.
Kenya ilipigwa marufuku na FIFA kujihusisha na soka baada ya Serikali kuingilia Shirikisho la Soka Kenya (FKF) Februari 25 ila ilijumuishwa kwenye makundi kwa matumaini zuio lingeweza kuondolewa. Kenya ilikuwa kundi C na timu za Cameroon, Namibia na Burundi ambazo sasa zitabaki tatu.
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT