Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Dkt. Kizza Besigye alikamatwa siku ya Jumanne alipokuwa akijaribu kuongoza maandamano katika mji mkuu, Kampala, kupinga gharama kubwa ya maisha.
–
Besigye mwenye umri wa miaka 66 aligombea urais dhidi ya Yoweri Museveni mara nne. Aliwahi kuwa daktari wa kibinafsi wa Rais Yoweri Museveni na amekamatwa mara nyingi.
–
Dkt Besigye alifika kwenye maandamano ya Jumanne akiwa na megaphone kwenye gari lake na kusimamisha shughuli za biashara katika eneo hilo.
–
Polisi wa Uganda waliambia shirika la habari la Reuters kwamba wanamshikilia Dkt Besigye kwa tuhuma za kuchochea ghasia.