Na Victoria Godfrey
Uongozi wa Bullet Force umem tangaza Athuman Idd Chuji kuwa kocha MKuu wa Klabu ya Bullet Force .
Chuji atakinoa kikosi hicho kinachojiandaa kushiriki mashindano ya Ndondo Cup msimu huu.
Akizungumza na waandishi wa Habari baada ya kutambulishwa Chuji,amesema waamejipanga kwenda kushindana na sio kushiriki
Amesema maandalizi yapo vizuri na wachezaji Wana morali ya hali ya juu.
“Tukishirikiana na benchi la ufundi tumejipanga vyema kwani si kwetu Kila mchezo ni fainali na tutakwenda uwanjani kupata matokeo,” amesema Chuji.
Naye Nahodha wa timu hiyo Yohana Mkomola, amesema maandalizi yapo vizuri na timu ipo kambini .
Amesema kuwa malengo yao kufanya vizuri hatua ya awali ili kufuzu hatua nyingine na kucheza fainali.
Kwa upande wa Meneja wa timu hiyo Catherine Mwakyusa, amesema wamejipanga kutwaa Ubingwa msimu huu.
Timu hiyo itaanza mchezo wake wa kwanza itavaana dhidi ya Saratoga fc katika mchezo utakaopigwa Juni 2 mwaka huu kwenye Uwanja wa Tandika.