Kikosi cha KMC FC kesho kitashuka katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC soka Tanzania bara dhidi ya Mbeya City utakaopigwa saa 16:00 jioni.
–
Timu hiyo ya Manispaa ya Kinondoni chini ya kocha Mkuu Thierry Hitimana itakuwa nyumbani ikimkaribisha Mbeya City na kwamba maandalizi ya mchezo huo yamekamilika kwa asilimia kubwa na hivyo Timu ipotayari kwa mtange huo.
–
Licha ya mchezo huo kuwa na ushindani mkubwa , lakini KMC imejipanga vizuri kutumia uwanja wanyumbani ilikupata matokeo mazuri na hivyo kuendelea kujiimarisha zaidi kwenye msimamo wa Ligi kuu ya NBC ambapo kwa sasa ipo katika nafasi ya nane.
Aidha katika mchezo huo wa kesho KMC itakosa huduma ya wachezaji wawili ambao ni Nickson Kibabage kutokana na mambo ya kifamilia pamoja na Charles Ilamfya mwenye kadi tatu za njano.
–
Kwaupande wa Afya za wachezaji ziko vizuri ,wanahari na morali nzuri na kwamba wachezaji pamoja na benchi la ufundi wamejiandaa kuwapa burudani mashabiki na Watanzania wote ambao siku zote wamekuwa wakiisapoti katika hali yoyote pindi inapokuwa uwanjani.
–
“Tunakwenda kwenye mechi ngumu pamoja na kwamba tutakuwa nyumbani ,tunaiheshimu Mbye City kwakuwa ni wazuri, wanawachezaji wazuri, lakini KMC tukobora zaidi kuhakikisha alama tatu muhimu zinabaki kwenye Manispaa yetu ya Kinondoni.
–
Hata hivyo katika mchezo uliopita duru ya kwanza uliopigwa kwenye uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya, timu zote mbili zilitoka zare ya mabao mawili kwa mawili ambapo magoli ya KMC yalifungwa na Matheo Anton pamoja na Mohamed Samata.
Imetolewa leo Mei 18
Na Christina Mwagala
Afisa Habari na Mawasiliano KMC FC.