Kocha wa klabu ya Coastal Union, Juma Mgunda kwa mara nyingine tena amelalamikia ratiba ya kucheza mechi katika muda wa Saa 8 mchana huku akisema kucheza muda huo ni adhabu ila hawawezi kugomea maana muda umepangwa kikanuni.
ADVERTISEMENT
–
Mgunda amesema “Mchezo wa mpira saa 8 mchana sio muda mzuri,yani kucheza mpira saa 8 ni adhabu. Kwa hiyo tumecheza mpira kwenye adhabu ya saa nane na tunamshukuru Mungu tumepata matokeo ya ushindi.Huu muda ni umepangwa kikanuni hivyo hatuwezi kugomea”
ADVERTISEMENT