BloombergUK Imeripoti, Majaji watatu nchini Uingereza wamesema kwa pamoja kuwa ‘Kutumia neno KIPARA Kama njia ya Kumwita au Kumtambua Mtu ni zaidi ya Kejeli, Ni UNYANYASAJI Wa KIJINSIA’.
–
Majaji hawa ambao pia wanavipara walikuwa wakihitikisha kesi ya Madai ya Fidia ya fundi umeme Tony Finn dhidi ya muajiri wake ambaye alimfukuza kazi baada ya miaka 24 ya utumishi bila kosa lolote na kumtukana kuwa yeye ni ‘Mtu Mnene Mwenye Kipara’.
–
Majaji hawa wamesema Kutumia Neno KIPARA Dhidi ya mtu ni ‘Unyanyasaji kama wa Kingono na Ubaguzi sababu maneno hayo yalisemwa kwa madhumuni la kutishia, kutukana, kudhalilisha na kuudhi Mtu ukizingatia kukosa nywele kwa wengi sio jambo la kujitakia’.