Liverpool wanataka uchunguzi ufanyike kuhusu sababu zilizopelekea mchezo wa wa Fainali wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya (UCL0 kuchelewa kuanza huku wakisisitiza kuwa jambo hilo hakikubaliki.
–
Ratiba ya awali ya mchezo huo ilipangwa saa 4:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki lakini mchezo huo ulianza saa 4:36 usiku.
–
Mchezo huo ulichelewa kuanza zaidi ya dakika 30 huku masuala ya kiusalama yakitajwa kuwa ni sababu. Mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Stade de France jijini Paris ilimalizika kwa Liverpool kupoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Real Madrid.