Klabu ya Liverpool imegomea ombi la klabu ya Fulham la kumchukua kwa mkopo winga mpya Fabio Calvalho kwa ajili ya msimu ujao.
–
ADVERTISEMENT
Jurgen Klopp anataka winga huyo raia wa Ureno kuwa sehemu ya kikosi chake msimu ujao na amesema anaweza kuwa mchezaji muhimu muda sio mrefu.
–
Liverpool imemsajili winga huyo mwenye umri wa miaka 19 kwa ada ya uhamisho inayotajwa kuwa pauni milioni 8.
–
ADVERTISEMENT
Calvalho amesaini mkataba wa miaka mitano na atajiunga rasmi na Majogoo hao Julai Mosi. Calvalho alifunga magoli 10 na kuisaidia kuirejejesha klabu hiyo kunako ligi kuu England.