Idadi ya visa vya maambukizo ya homa ya nyani imepanda nchini Uingereza baada ya taifa hilo kuthibitisha kuwa watu wengine 11 wameambukizwa maradhi hayo yanayababishwa na virusi kutoka kwa wanyama wa porini.
–
Waziri wa Afya wa Uingereza Sajid Javid amesema visa hivyo vipya vinafuatia vingine 9 ambavyo Uingereza ilikwisharipoti hapo kabla na amearifu kuwa wengi ya wagonjwa waliobainika hawana maambukizi ya kutisha.
–
Ujerumani nayo imetangaza kugundulika kisa cha kwanza cha ugonjwa huo ambao husambaa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine kupitia njia ya hewa, majimaji ya mwilini au kutumia vifaa vya mtu aliyeambukizwa.
–
Mataifa mengine ikiwemo Ufaransa, Canada, Marekani, Ureno, Uhispania, Ubelgiji , Italia, Sweden na Australia pia yamethibitisha kuwa na visa kadhaa vya homa hiyo iliyogundulika kwa mara ya kwanza duniani mnamo mwaka 1970.