Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama barabarani limetangaza kiama kwa madereva sugu wenye kuvunja sheria za barabarani kwa makusudi na kusababisha ajali.
–
Hayo yameelezwa Mei 14, 2022 mjini Geita na Kamanda wa Polisi Kitengo cha usalama barabarani nchini, Kamishina Msaidizi mwandamizi, Wilbroad Mutafungwa katika mwendelezo wa Oparesheni ya wa ukaguzi wa vyombo vya usafirishaji.
–
Mutafungwa amesema jeshi litawafungia leseni zao pamoja na kuwafikisha Mahakamani madereva wote wenye kujitia kiburi na usugu wa kutotii sheria.
–
Katika ufafunuzi wake mtafungwa amesema operesheni ya mwezi mmoja ya ukaguzi wa vyombo vya moto imekamata jumla ya makosa 38,276 ya waendesha pikipiki, makosa ya bima ya Magari (6769) na bima za pikipiki ( 6,520) makosa ya kutokuvaa kofia ngumu (9,931) Ulevi 494, kuzidisha abiria Magari (9,107) kuzidisha abiria mshikaki (7,590) huku jumla ya Magari yote Ni 128,014 yalikaguliwa Katika kipindi chote Cha msako huo maalumu nchi Nzima.
–
Nao baadhi ya Madereva pamoja na abiria wamelishukuru jeshi la polisi kwa msako huo ambao utapunguza ajali kwa wingi.