Mchezaji wa klabu ya Manchester United na England, Harry Maguire amefunga ndoa ya kimya kimya Serikalini na mpenzi wake wa muda mrefu Fern Hawkins.
–
Ndoa hiyo imefungwa katika ofisi za Crewe Registry na ilihudhuriwa na watu wachache sana wakaribu wakiwemo wazazi wa Maguire.
–
Maguire na mkewe wanatarajia kufanya shughuli kubwa ya harusi mnamo mwezi Juni nchini Ufaransa.