ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Wednesday, June 29, 2022
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

MAJALIWA: WANAOTOA ARDHI WALIPWE FIDIA

Ally Hamis Zingizi by Ally Hamis Zingizi
May 27, 2022
in HABARI
0
MAJALIWA: WANAOTOA ARDHI WALIPWE FIDIA
0
SHARES
38
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameitaka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ihakikishe Watanzania wanaotoa ardhi yao waliyomilikishwa kihalali kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kimaendeleo ikiwemo uwekezaji wanalipwa fidia zao kwa wakati.

RelatedPosts

R KELLY AHUKUMIWA MIAKA 30 JELA

R KELLY AHUKUMIWA MIAKA 30 JELA

Jun 29, 2022

POLISI 156 WAFUKUZWA MAFUNZONI

Jun 29, 2022

VIGOGO WA CHAMA CHA WALIMU WAHUKUMIWA MIEZI 6 JELA

Jun 29, 2022
Load More

Amesema hayo leo (Alhamisi, Mei 26, 2022) wakati akijibu swali la Mbunge wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu. Mbunge huyo alitaka kujua Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha wananchi ambao maeneo yao yamechukuliwa na wawekezaji wanalipwa fidia.

Amesema ni muhimu kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuendelea kusimamia ulipwaji wa fidia kwa wananchi waliotoa ardhi zao kwa shughuli za kimaendeleo. ”Nikuhakikishie Mheshimiwa Mbunge kama kuna madai yametolewa na hasa kama uthamini umefanyika basi thamani ya ile ardhi iliyochukuliwa kwa ajili ya kupisha shughuli nyingine ni lazima fidia ilipwe ili haki itendeke”

Akijibu Swali ya Mbunge wa Moshi Mjini, Priscus Tarimo aliyetaka kujua mpango wa Serikali wa kupima maeneo ya Miji, Manispaa na Jiji, Waziri Mkuu amesema kuwa mpango huo ni endelevu wenye lengo la kupima maeneo yote nchini ili kubainisha huduma zote zinazotakiwa kutumika katika ardhi hiyo.

Mheshimiwa Majaliwa ameongeza kuwa mpango huo utakwenda hadi maeneo ya vijijini ili kuwasiaidia kupata maeneo yaliyopimwa na kutambulika rasmi ili waweze kupata hati. “Tunataka watumie hati hizi kama mtaji wa kukopea kwenye taasisi zetu za fedha, lengo ni kila Mtanzania anufaike na ardhi iliyopo, hivyo Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi iendelee kukamilisha zoezi hili, hii itawasaidia hata wawekezaji kutambua maeneo ya uwekezaji”

Wakati huohuo, Waziri Mkuu amesema kuwa Serikali imeendelea kuhamasisha wakulima wadogo wa chikichi waendelee kulima kwa wingi zao hilo lengo likiwa ni kuhakikisha nchi inazalisha kwa wingi mafuta ya kula.

Pia, Mheshimiwa Majaliwa ametoa wito kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuwekeza kwenye kilimo hicho kwa kuwa nchi ina ardhi ya kutosha na yenye rutuba. “Ardhi tunayo, na tumeshatoa maagizo kwa wakuu wa mikoa wote kutenga ardhi kwa ajili ya uwekezaji”

“Tunataka tuzalishe na tukamue mafuta yetu sisi wenyewe, tunaamini gharama itakuwa ndogo na zile fedha tunazotumia kuagiza mafuta nje hazitakwenda tena bali tutaziingiza kwenye shughuli nyingine za kimaendeleo, uwekezaji huu ni mkubwa na endelevu”

ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT

Alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Kigoma Kaskazini Assa Makanika ambaye alitaka kujua mkakati wa Serikali wa kuwakaribisha wawezaji wakubwa ili kupunguza Nakisi ya kuagiza mafuta ya kula nchini.

Mheshimiwa Majaliwa aliongeza kuwa, Serikali imeweka mkakati wa kuhakikisha inaimarisha teknolojia inayotumika katika kukamua mafuta ya chikichi “Sasa tunakwenda kuimairisha viwanda vya ukamuaji ili tuweze kukamua asilimia 99 ya mafuta kwenye chikichi badala ya 70 ya sasa”

Related

ADVERTISEMENT
Ally Hamis Zingizi

Ally Hamis Zingizi

Related Posts

R KELLY AHUKUMIWA MIAKA 30 JELA
HABARI

R KELLY AHUKUMIWA MIAKA 30 JELA

by Shabani Rapwi
Jun 29, 2022
POLISI 156 WAFUKUZWA MAFUNZONI
HABARI

POLISI 156 WAFUKUZWA MAFUNZONI

by Shabani Rapwi
Jun 29, 2022
VIGOGO WA CHAMA CHA WALIMU WAHUKUMIWA MIEZI 6 JELA
HABARI

VIGOGO WA CHAMA CHA WALIMU WAHUKUMIWA MIEZI 6 JELA

by Shabani Rapwi
Jun 29, 2022
MAHAKAMA YATOA AMRI KESI HALIMA MDEE NA WENZAKE
HABARI

MAHAKAMA YATOA AMRI KESI HALIMA MDEE NA WENZAKE

by Shabani Rapwi
Jun 29, 2022
RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI HUU
HABARI

RAIS SAMIA ATEUA MKUU WA MAJESHI YA ULINZI

by Shabani Rapwi
Jun 29, 2022
MPOLE AMFUNIKA MAYELE LIGI KUU YA NBC 2021/22
HABARI

MPOLE AMFUNIKA MAYELE LIGI KUU YA NBC 2021/22

by Shabani Rapwi
Jun 29, 2022

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
May 2022
M T W T F S S
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031  
« Apr   Jun »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In