Kocha Mkuu na Meneja wa klabu ya Mbeya Kwanza, Mbwana Makata na David Naftar wameliomba radhi Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi kwa tukio walilofanya na kusababishwa kufungiwa kwa miaka mitano kutojihusisha na soka.
–
“Natumia fursa hii kuwaomba radhi TFF, Bodi ya Ligi, wadhamini wetu NBC na Azam Media” maneno ya kocha wa Mbeya Kwanza Mbwana Makata akiungana na meneja David Naftari kuomba radhi baada ya kufungiwa miaka mitano na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania.
–
Wawili hao walifungiwa baada ya klabu ya Mbeya Kwanza kugomea kucheza dhidi ya Namungo FC dimbani Ilulu Lindi kwa madai ya kutokuwepo gari la kubebea wagonjwa (Ambulance).