ADVERTISEMENT
Manchester City imezindua sanamu la nguli wa soka wa klabu hiyo Sergio Kun Aguero katika kumbukumbu kuadhimisha miaka 10 ya goli la Muargentina huyo lililopatia Man City ubingwa wa Ligi kuu England mnamo 2012.
–
Mnamo Mei 13, 2012 Man City ilitwaa kombe la Ligi kuu England kwa namna ya kipekee baada ushindi wa dakika za lala salama wa 3-2 dhidi ya Queens Park Rangers na kuipiku Man United wakiwa na alama sawa City ikiongoza kwa utofauti wa magoli.
–
Katika mechi za duru ya kufunga pazia la msimu wa 2011/12 wa #EPL Man City ilikuwa na kibarua dhidi ya QPR huku Man United ikizichapa dhidi ya Sunderland zote zikiwa na alama 86.
–
Man United ilipata uongozi mapema mnamo dakika ya 20 kupitia kwa naam! umeotea Phil Jones goli ambalo lilidumu mpaka mwisho wa mchezo.
–
Man City ilipata uongozi kupitia kwa Pablo Zabaleta 39′ (assist Yaya Toure) na kwenda mapumzikoni vifua mbele 1-0 kabla ya QPR kucharuka kipindi cha pili na kupata uongozi kupitia magoli ya Djibril Cisse 48′ na Jamie Mackie 66′ licha ya Joey Barton 55′ kula umeme.
–
Mpaka dakika ya 90′ QPR iliyokuwa pungufu ya mchezaji mmoja ilikuwa inaongoza 2-1 dhidi ya Man City huku mashabiki wa Mashetani Wekundu wakiomba Dua matokeo yabaki hivyo ili wachukue kombe lao 20 la Ligi kuu England.
–
Mnamo dakika ya 90+2′ Edin Dzeko (assist David Silva) aliisawazishia Man City 2-2 kabla ya Sergio Kun Aguero (assist ya Balotelli) kufunga goli ambalo lilileta simanzi huko Old Trafford na kwa mashabiki wa Manchester United ulimwenguni kote.
–
Roberto Mancini na vijana wake walitwaa kombe hilo kwa mara ya kwanza kihistoria kwa matokeo ya 3-2 dhidi ya QPR baada ya kufikisha alama 89 sawa na Manchester United ikiwa na utajiri wa utofauti wa magoli.
ADVERTISEMENT