Msemaji wa Yanga, Haji Manara amejibu mchambuzi wa Wasafi FM, George Job aliedai kuwa Yanga SC ni bora kwa sababu ya Aanguko la Simba SC.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ameandika 

“Ndugu yangu Mchambuzi mahiri,,nna maswali kidogo juu ya kauli yako hii. Makolo walipokuwa Mabingwa Kwa misimu minne mfululizo,,Je Yanga nayo ilikuwa na anguko? Au Wakishinda Wananchi ni kwa sababu wao wameanguka? Wameanguka kivipi wakati juzi tu walikuwa wanacheza Robo fainali ya Afrika? ( sio Shirikisho).
–
Wameanguka vipi wakati ni Mabingwa wa Mapinduzi? Wameanguka vp wakati majuzi tu mlikuwa mnasema Yanga wawaige Makolo? Mlikuwa mnatuchuuza sio tuwaige walioanguka? Guys, hii Kwa sasa haiwezi kuwasaidia na mnapaswa kuukubali ukweli mchungu kwamba, Yanga imeboresha kikosi chake, Wachezaji wapya na ukichanganya wale waliobaki, kumeleta matokeo chanya uwanjani..
–
Maingizo ya kina @ybangalaa4 , @mayelefiston ,@auchokhalidofficial @djiguidiarraofficial ,@sure8boy na wengine wapya kumeimarisha hii team,,plus na kina @feisal194 @bakarmwamnyeto_03 , @jobdick05 , @ntibazonkizasaidi , @kibwana_shomari na wengine wa zamani,,kumefanya @yangasc iwe very strong ndani ya Pitch. Suala la eti Makolo Wameanguka ndio maana Yanga kawa bora ,. it’s not true at all, mbona hamkusema hayo wao walipokuwa Mabingwa? Wakishinda wao wanajua ila akishinda Yanga ni kwa sababu wao Wameanguka? kubalini investment ya uwanjani iliyofanywa na GSM, mengine mtaonekana Washabiki tu.
–
YANGA imetwaa ubingwa mara 27,,mara nyingi zaidi kuliko Club yoyote nchi hii,,,miaka yote hyo kulikuwa na anguko la Makolo? Tuwe serious kidogo, na tuheshimu team nyingine hata kama tunataka kuufanya ubingwa wao hauna maana. Imagine Two years back Yanga alikuwa anachukua Points Nne ktk ligi kuu,,msimu huu tumechukua mbili tu, why ianguke mwaka huu na isiwe Miaka miwili nyuma?
–
Dogo, umeikosea heshma inayostahili Yanga, hukusimama na ukweli na umetaka kuonyesha ubingwa wetu ni kutokana na ubovu wao ,,ila bad luck huna facts hata mmoja, Kiufupi andiko lako limejaa ushabiki. Yaani Umesahau Bakuli la Wananchi miaka michache nyuma? Isiwe Yanga ndio ilikuwa na anguko iwe leo kwa Simba waliowekeza Bilioni shirini za mchongo? By the way hata ikianguka,,Hzo sio SHEEDA ZETU, waanguke au wateleze cc HAITUHUSU”
ADVERTISEMENT