Dereva wa langalanga (Formula 1) Max Verstappen wa Red Bull, ameshinda taji lake la tatu msimu huu baada ya kufanikiwa kumaliza nafasi ya kwanza kwenye michuano ya Miami Grand Prix.
–
Nafasi ya pili imekamatwa na mpinzani wake wa karibu Charles Leclerc na nafasi ya tatu imeenda kwa Carlos Sainz wote ni kutoka Kampuni ya Ferrari.
–
Kwa upande wake bingwa mara saba wa Langalanga, Lewis Hamilton alimaliza nafasi ya sita huku akiachwa na mwenzake wa Mercedes, George Russell aliyemaliza nafasi ya tano.
–
Max ameshinda kila taji msimu huu ambapo alifanikiwa kumaliza mbio hadi mwisho, mara mbili alizokosa (Bahrain GP & Australian GP) hakuweza kumaliza hadi mwisho kufuatia tatizo kwenye injini ya gari (Red Bull).