Shirikisho la soka Nchini Ghana limemfungia mchezaji wa Asante Kotoko, Richmond Lamptey kujihusisha na masuala ya soka kwa kipindi cha miezi 30 kwa kuhusika katika upangaji wa matokeo wakati akiwa klabu ya Inter Allies.
–
Sambamba na hilo wachezaji wengine kadhaa wa klabu ya Inter Allies pia wamefungiwa.
–
Aidha klabu ya Inter Allies huenda ikashushwa mpaka ligi daraja la pili kwa kukutwa na hatia ya upangaji wa matokeo katika mchezo wa mwisho wa msimu uliopita dhidi ya AsantiGold.