ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Friday, March 24, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

MELI KUBWA YA MAGARI 4397 YAWASILI BANDARI YA DAR ES SALAAM, YAVUNJA REKODI…!

I am Krantz by I am Krantz
May 9, 2022
in HABARI
0
MELI KUBWA YA MAGARI 4397 YAWASILI BANDARI YA DAR ES SALAAM, YAVUNJA REKODI…!
0
SHARES
234
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT

Meli kubwa ya shehena ya magari inayojulikana kama Meridian ACE ikiwasili katika Bandari ya Dar es Salaam.

Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Bw. Nicodemas Mushi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA, mara baada ya kuwasili kwa meli hiyo.


Meli kubwa ya shehena ya magari inayojulikana kama Meridian ACE ikiwasili katika Bandari ya Dar es Salaam.


Muonekano wa mbele wa Meli ya Meridian ACE ikiwasili katika Bandari ya Dar es Salaam leo mchana.


Muonekano wa nyuma wa Meli ya Meridian ACE ilipokuwa ikiwasili katika Bandari ya Dar es Salaam leo mchana.

MELI kubwa ya shehena ya magari yapatayo 4397 imewasili katika Bandari ya Dar es Salaam. Meli hiyo ya MERIDIAN ACEyenye idadi kubwa ya magari imewasili leo majira ya saa sita mchana na kuvunja rekodi, ikiwa na idadi kubwa ya magari kuwasili kwa mara moja katika Bandari hiyo. 

Akizungumza na vyombo vya habari kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Bw. Eric Hamis, Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa TPA, Bw. Nicodemas Mushi alisema wanayofuraha kubwa kuipokea meli ya Meridian ACE, iliyovunja rekodi ya nyumba iliyowekwa mwezi mmoja uliopita ya kuwasili magari 4o41  mwezi Aprili 8, 2022.

RelatedPosts

BABA MWENYE NYUMBA AFUMANIWA NA MKE WA MPANGAJI WAKE

BABA MWENYE NYUMBA AFUMANIWA NA MKE WA MPANGAJI WAKE

Mar 24, 2023

WANAOKULA HADHARANI MCHANA WA RAMADHANI KUKAMATWA

Mar 24, 2023

HII KALI : KUISHI CHINI YA MAJI SIKU 100 KISA KUTAFUTA REKODI HII

Mar 24, 2023
Load More

Akifafanua zaidi, Bw. Mushi alisema meli hiyo imetokea nchini Japan na kupitia nchini Singapore na kuja moja kwa moja katika Bandari ya Dar es Salaam. “Kama ambavyo tumeshuhudia meli hiyo imetuletea magari 4397, huku asilimia 23 yaani magari 991 yatabaki nchini Tanzania na asilimia 77 yatakwenda nje ya nchi. 

Aliongeza kuwa magari yaliyosalia yanatarajiwa kupelekwa katika nchi za Zambia, Malawi, Rwanda, Burundi pamoja na DR Congo.

ADVERTISEMENT

“Niseme kwamba hii ni hatua muhimu inayoonesha imani ya Watanzania, wateja na wadau wengine wa ndani na nje ya nchi, ambao kutokana na ubora wa kazi inayofanyika na imani ya wateja wetu kwenye eneo la ulinzi na usalama, ubora wa huduma pamoja na umakini unaofanyika katika utoaji wa huduma hizi. 

Aidha alisema kuwasili kwa meli hiyo kuna maana kubwa katika uchumi wa Tanzania, kwani ujio wa meli kubwa kama Meridian Ace ni ishara ya ufanisi mkubwa wa Bandari ya Dar es Salaam. Alibainisha kuwa ili kuweza kupata makampuni makubwa na mawakala wakubwa wenye mzigo kama huo ni lazima pawepo na imani ya watumiaji wa Bandari.

Alisema ujio wa meli hiyo ni jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake za uboreshaji shughuli za bandari na uwekezaji mkubwa wa vifaa ambayo vimewekwa ili kuboresha huduma na ufanisi wa kazi bandarini. 

“…Mfano ujenzi wa miundombinu, ununuzi wa vifaa vya kazi, vyote hivi vinaifanya bandari yetu sasa kutoa huduma katika kiwango cha juu kabisa cha ubora, itakumbukwa kwamba katika eneo la ulinzi na usalama tunafanya vizuri sana. 

ADVERTISEMENT

“Mizigo ya wateja wetu yote inafika katika ubora na inaondoka bandarini kwetu ikiwa salama kabisa, habari hizi njema zinawafanya wateja wapya pamoja na wasiku zote kuendelea kuiamini bandari yetu…ikumbukwe kwamba menejimenti ya TPA ikiongozwa na Bodi ya Wakurugenzi pamoja na ushauri na ulezi makini kutoka Wizara yetu Mama Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi…,” alisisitiza.

“…Tunafanya kampeni kubwa za kimasoko ndani ya nchi pamoja na nje ya mipaka ya Tanzania lengo likiwa ni kutumia fursa zote zinazotuzunguka kuanzia nchi zote majirani zetu zinapitisha mzigo kupitia Bandari ya Dar es Salaam nchini Tanzania.” Alisema Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa TPA, Bw. Mushi mara baada ya kuwasili kwa meli hiyo.

Related

ADVERTISEMENT
I am Krantz

I am Krantz

👉 FOUNDER & CEO of KONCEPT 👉Serial & Self-made Entrepreneur 👉Digital media consultant 👉Pr & media Guru/Awards winner Blogger 👉Startuper of the year 2016 by TOTAL 👉TOP 50 Most influential young Tanzania 2017 👉General Secretary at Tanzania Bloggers Network 👉 UPG Sustainability Leader in the Class of 2021 👉 ALUMNI The Tony Elumelu Foundation 👉Chairman YOUNG CEO CLUB Tanzania 🇹🇿 ‘ 😊 Marketer BY Education, Entrepreneur BY Profession & Blogger BY Passion ”😊

Related Posts

BABA MWENYE NYUMBA AFUMANIWA NA MKE WA MPANGAJI WAKE
HABARI

BABA MWENYE NYUMBA AFUMANIWA NA MKE WA MPANGAJI WAKE

by Shabani Rapwi
Mar 24, 2023
WANAOKULA HADHARANI MCHANA WA RAMADHANI KUKAMATWA
HABARI

WANAOKULA HADHARANI MCHANA WA RAMADHANI KUKAMATWA

by Shabani Rapwi
Mar 24, 2023
HII KALI : KUISHI CHINI YA MAJI SIKU 100 KISA KUTAFUTA REKODI HII
HABARI

HII KALI : KUISHI CHINI YA MAJI SIKU 100 KISA KUTAFUTA REKODI HII

by Shabani Rapwi
Mar 24, 2023
WANAUME WANAONYANYUA VITU VIZITO WATAJWA RIJALI ZAIDI
HABARI

WANAUME WANAONYANYUA VITU VIZITO WATAJWA RIJALI ZAIDI

by Shabani Rapwi
Mar 24, 2023
MWALIMU JELA MIAKA 30 KWA KUMLAWITI MWANAFUNZI
HABARI

MWALIMU JELA MIAKA 30 KWA KUMLAWITI MWANAFUNZI

by ALFRED MTEWELE
Mar 24, 2023
BENKI YA NBC YAZINDUA KAMPENI YA MKEKA WA USHINDI NA ATM ZA NBC
HABARI

BENKI YA NBC YAZINDUA KAMPENI YA MKEKA WA USHINDI NA ATM ZA NBC

by I am Krantz
Mar 24, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
May 2022
M T W T F S S
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031  
« Apr   Jun »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In