Aliyekuwa Mgombe Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020, kupitia Chama cha ACT Wazalendo, Bernard Membe ameeleza sababu zilizomfanya arejee CCM ikiwemo kutokuwepo tena kwasababu ambayo ilimfanya atimkie upinzani “Sababu zilizonifanya niondoke CCM hazipo tena”
–
Membe amefunguka jinsi alivyoumia kutokana na uamuzi wa kumwondolea uanachama wa CCM, Chama alichokulia huku akiahidi sasa atafia ndani ya CCM.
–
Akizungumza katika mkutano huo uliofanyka leo katika Kijiji cha Chiponda Mkoani Lindi amesema “Nimerejea CCM kwa sababu kuu mbili, sababu ya kwanza nilishauriwa na viongozi wa dini zote, nilishauriwa na viongozi wa CCM ngazi ya Wilaya na Mkoa, nilishauriwa na marafiki zangu wote nirejee CCM, nilishauriwa na wana CCM.
–
“Sababu ambazo zilinifanya niondoke CCM haziko tena, narudi sababu zilizoniondoa CCM haziko tena, nimerudi namshukuru Mwenyekiti wa CCM na wajumbe wa Kamati Kuu kunirudisha, nimerudi kwenye Chama ambacho nimezaliwa na kukulia, chama ambacho kimenisomesha, sitoondoka tena”