Watu 27 wamefariki dunia na wengine 12 kujeruhiwa baada ya moto kutokea katika jengo lenye ghorofa nne Jijini Delhi Nchini India, Polisi wamesema kulikuwa na watu zaidi ya 70 katika jengo hilo.
–
Zaidi ya mashine 20 zilitumika kupambana kuuzima moto huo, ambapo watu wawili wanashikiliwa na mamlaka za usalama. Inadaiwa chanzo ni shoti ya umeme kwa kuwa jengo halikuwa na miundombinu mizuri ya umeme.
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT
–
Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi ametoa pole na kuahidi kutoa Dola 2,580 (Tsh milioni 5.9) kwa kila familia iliyopoteza ndugu katika tukio hilo.