ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Monday, March 20, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

MPANGO WA KUINUA UFAULU MASHULENI (PIP) WA BARRICK BULYANHULU WAZIDI KUPATA MAFANIKIO NYANG’HWALE

I am Krantz by I am Krantz
May 4, 2022
in HABARI
0
0
SHARES
183
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT

RelatedPosts

RJ THE DJ VIFO VINAONGEZA MSONGO WA MAWAZO

ROMY JONS AOMBA MSAMAHA

Mar 20, 2023

MCHUNGAJI AFUNGA KANISA KISA ASHINDA MIL 100 ZA “KUBETI”

Mar 20, 2023

WAZIRI BITEKO ATAKA BAJETI YA 2023/24 KUZINGATIA VIPAUMBELE VYA WIZARA

Mar 20, 2023
Load More

Meneja wa Mahusiano ya Kijamii wa Barrick Bulyanhulu, Agapiti Paul akiongea kuhusu mafanikio ya mpango wa kuongeza Ufaulu

***
Mpango wa kuinua ufaulu shuleni (Performance Improvement Program (PIP) unaotekelezwa na kampuni ya Barrick kupitia mgodi wa Bulyanhulu, kwa kushirikiana na Halmashauri ya Nyang’hwale iliyopo mkoani Geita, umefanikiwa kupata matokeo mazuri kwa kuongeza idadi ya ufaulu wa wanafunzi wilayani humo.

 Kabla ya kuanzishwa mpango huu unaolenga shule za sekondari ufaulu wa wanafunzi wa kidato cha nne wilayani humo kwa kiwango cha daraja la kwanza ulikuwa wa wanafunzi watano kwa sasa idadi imeongezeka kufikia wanafunzi 55.

Hayo yamebainishwa wakati wa hafla ya kuwatukia zawadi wanafunzi kutoka shule mbalimbali waliofaulu vizuri sambamba na walimu waliofanikisha ufaulu huo kupitia programu hii ya (PIP).

 Mgeni rasmi katika hafla hiyo iliyofanyika wilayani humo na kuhudhuriwa na Walimu, wazazi, wanafunzi na wafanyakazi wa Barrick alikuwa ni Mkuu wa wilaya hiyo, David Jamhuri

Progamu hii ilianzishwa mwaka 2019 kwa lengo la kuinua kiwango cha ufaulu kwa Wanafunzi wa shule za Sekondari na kupunguza utoro mashuleni hususani kwa Wasichana. Kutokana na matokeo chanya ya mpango huu kwa wanafunzi, Kamati ya Maendeleo ya Jamii (CDC) ya imekuwa ikitenga fedha kila mwaka ili kufanikisha utekelezwaji wake.

Meneja wa Mahusiano ya Kijamii wa Barrick Bulyanhulu, Agapiti Paul, alisema katika kipindi cha mwaka 2021 kampuni ilitenga kiasi cha shilingi milioni 50 kwenye bajeti ya miradi ya Kijamii (CSR) katika Halmashauri ya Nyang’hwale, kwa ajili kununua vitabu kwa ajili ya wanafunzi na walimu katika shule 10 za sekondari za Serikali wilayani humo, kutoa zawadi za motisha kwa wanafunzi waliofaulu kwa daraja la kwanza, wazazi wa wanafunzi hao, walimu ambao masomo wanayofundisha wanafunzi waliyafaulu vizuri na shule ambazo zimepata wanafunzi wenye ufaulu huo.

Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Nyang’hwale, David Jamhuri, alipongeza jitihada zinazofanywa na Barrick kutoa motisha kwa walimu na wanafunzi kwa lengo la kuongeza kiwango cha ufaulu wa wanafunzi wilayani humo, ”Naamini ushirikiano wa Serikali na Barrick kupitia mpango huu utaleta mafanikio makubwa zaidi, Natoa wito kwa walimu na wanafunzi kuongeza bidii wakati wote kufanikisha malengo ya Serikali ya kuboresha sekta ya elimu ya elimu nchini ambayo inazidi kuboresha miundo mbinu mashuleni na kukabili changamoto mbalimbali zilizopo”.alisema.

Mmoja wa wanafunzi aliyenufaika na mpango huu, Egide John Halalawe,kutoka sekondari ya Msalala akiongea kwa niaba ya wenzake alisema kupitia mpango huo wanafunzi wananufaika kwa kupata vitabu pia kupatiwa chakula shuleni na umewezesha walimu kufundisha kwa bidii na kusimamia kwa karibu wanafunzi wanapokuwa kwenye mwaka wa mtihani.

“Tunashukuru Barrick na Halmashauri kwa kubuni mpango huu, tuna imani utawezesha wanafunzi wengi kufanya vizuri zaidi katika mitihani yao ikiwemo kupata daraja la kwanza na madaraja mengine ya juu ya ufaulu”, alisema.

Akiongea kwa niaba ya wazazi, Idd John, alisema mpango huu ni mzuri na unahamasisha watoto kujituma zaidi pia wazazi wengi wasio na uwezo watoto wao wanasoma vizuri kutokana na kupatiwa vitabu vya kutosha sambamba na kupatiwa chakula mashuleni vilevile walimu wamekuwa wakifundisha wanafunzi waliopo kwenye mwaka wa mtihani wakati wa vipindi vya likizo bila kuhitaji malipo yoyote kutoka kwa wazazi.
Mkuu wa wilaya ya Nyang’hwale, David Jamhuri akiongea katika hafla hiyo
Egide John Halalawe,kutoka sekondari ya Msalala aliyepata daraja la kwanza katika mtihani wa kidato cha nne mwaka jana akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Nyang’hwale, David Jamhuri
Baadhi ya Walimu kutoka shule za sekondari zilizochangia kufanikiwa kwa mpango huu wakipokea zawadi za motisha kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Nyang’hwale, David Jamhuri.
Baadhi ya Walimu kutoka shule za sekondari zilizochangia kufanikiwa kwa mpango huu wakipokea zawadi za motisha kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Nyang’hwale, David Jamhuri.
Picha ya pamoja ya Watendaji wa Wilaya ,Barrick na walimu wakati wa hafla hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale, David Jamhuri akiendelea kuwatunza wanafunzi waliokuwa wakitoa burudani ya ngoma katika hafla hiyo.
Wanafunzi kutoka shule mbalimbali walihudhuria hafla hiyo
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT

Related

ADVERTISEMENT
I am Krantz

I am Krantz

👉 FOUNDER & CEO of KONCEPT 👉Serial & Self-made Entrepreneur 👉Digital media consultant 👉Pr & media Guru/Awards winner Blogger 👉Startuper of the year 2016 by TOTAL 👉TOP 50 Most influential young Tanzania 2017 👉General Secretary at Tanzania Bloggers Network 👉 UPG Sustainability Leader in the Class of 2021 👉 ALUMNI The Tony Elumelu Foundation 👉Chairman YOUNG CEO CLUB Tanzania 🇹🇿 ‘ 😊 Marketer BY Education, Entrepreneur BY Profession & Blogger BY Passion ”😊

Related Posts

RJ THE DJ VIFO VINAONGEZA MSONGO WA MAWAZO
HABARI

ROMY JONS AOMBA MSAMAHA

by Shabani Rapwi
Mar 20, 2023
MCHUNGAJI AFUNGA KANISA KISA ASHINDA MIL 100 ZA “KUBETI”
HABARI

MCHUNGAJI AFUNGA KANISA KISA ASHINDA MIL 100 ZA “KUBETI”

by ALFRED MTEWELE
Mar 20, 2023
WAZIRI BITEKO ATAKA BAJETI YA 2023/24 KUZINGATIA VIPAUMBELE VYA WIZARA
HABARI

WAZIRI BITEKO ATAKA BAJETI YA 2023/24 KUZINGATIA VIPAUMBELE VYA WIZARA

by Shabani Rapwi
Mar 20, 2023
TMA YATOA TAHADHARI MVUA KUBWA MIKOA HII KUANZIA LEO NA KESHO
HABARI

TMA YATOA TAHADHARI MVUA KUBWA MIKOA HII KUANZIA LEO NA KESHO

by Shabani Rapwi
Mar 20, 2023
WATU 5 WASHIKILIWA NA POLISI KWA TUHUMA WIZI MAFUTA SGR
HABARI

WATU 5 WASHIKILIWA NA POLISI KWA TUHUMA WIZI MAFUTA SGR

by ALFRED MTEWELE
Mar 20, 2023
MARUFUKU KUTOA FEDHA UPATE DHAMANA POLISI
HABARI

MARUFUKU KUTOA FEDHA UPATE DHAMANA POLISI

by Shabani Rapwi
Mar 20, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
May 2022
M T W T F S S
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031  
« Apr   Jun »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In