Mtanzania Rogers Kyaruzi (30) ameuawa kwa kupigwa risasi na Polisi jijini Atlanta nchini Marekani. Tukio hilo lilitokea katika Mgahawa wa Roasters Rotisserie Jumatano ya Mei 4.
–
ADVERTISEMENT
Kwa mujibu wa wafanyakazi wa Mgahawa huo na polisi, Rodgers alikuwa akiwasumbua wateja, ndipo polisi mmoja aliyekuwa maeneo ya karibu aliitwa, akafika na kumsihi Rodgers aondoke, lakini alikataa kutii amri ya polisi.
–
Hata hivyo dada yake Rodgers pamoja na rafiki zake wamesema kuwa kwa jinsi walivyomfahamu Rodgers maelezo hayo hayaeleweki. Uchunguzi bado unaendelea
ADVERTISEMENT