Mufti mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir leo Mei Mosi, 2022 ametangaza kuwa waislamu wote nchini watapaswa kuendelea na mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa kuwa mwezi haujaandama.
–
Sheikh Abubakar Zubeir amesema Sikukuu ya Eid itakuwa Jumanne ya Mei 03, 2022 ambapo amebainisha kuwa Baraza la Eid litafanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere na Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais Samia Suluhu Hassan.
ADVERTISEMENT