Chuo kimoja katika jimbo la Sokoto kaskazini magharibi mwa Nigeria kimefungwa kwa muda usiojulikana baada ya Mwanafunzi wa kike chuoni hapo kuuawa kwa madai ya kukufuru dini ya kiislamu.
–
Mwanafunzi huyo ambaye jina lake halijatajwa alishtakiwa kwa kumtusi Mtume Muhammad jambo ambalo lilisababisha baadhi ya Wanafunzi waislamu kumshambulia na kumchoma moto na kusababisha kifo chake ndani ya eneo la Chuo, Alhamisi.
–
Gavana wa jimbo la Sokoto Aminu Tambuwal aliamuru kufungwa kwa chuo hicho na kuagiza Wizara ya elimu ya juu na Vyombo husika vya usalama kuchunguza tukio hilo na kuwataka Watu wa jimbo hilo kuwa watulivu na kudumisha amani kwani Serikali itachukua hatua zinazofaa kuhusu matokeo ya uchunguzi.