Mwanadada Oksana raia wa Ukraine ambaye kitaaluma ni nesi, alilipukiwa na bomu wakati akiwa anawatibu wanajeshi wa Ukraine waliojeruhiwa vitani na majeshi ya Urusi.
–
Bomu hilo likasababisha akatike miguu yote miwili na vidole vinne vya mkono wa kulia, akalazwa hospitali ambako bado anaendelea na matibabu.
–
Kabla hajafikwa na mkasa huo, alikuwa kwenye penzi zito na mwanaume aitwaye Victor ambaye pia ni raia wa Ukraine ambaye aahadi kufunga pingu za maisha.
–
Siku chache zilizopita, Victor ameenda kutimiza ahadi yake kwa kumuoa Oksana akiwa wodini, tena akiwa hana miguu, Akafanikiwa ahadi yake na kumfanya Oksana atabasamu tena kwa furaha.