1. MATUSI NA MAJIGAMBO
Usinibabaishe babu kama wewe unajisaidia wima basi mie nachutama tusitishane. Kama mama yako hajakufunza basi mie ndio mwalimu mkuu kwangu utasoma kwa lazima. Kauli hizi hafai kuolewa.
–
2. LAWAMA NA GUBU
Kuna shoga yangu kanunua iphone basi na mimi ninunulie kama kweli unanipenda na unataka kunioa. Haridhiki na anachopewa hata kidogo tupa mbali hafai kuwa mke.
–
3. HANA HESHIMA NA WAZAZI WAKO
Mie ukinioa sitaki wazazi wako wawe wanakuja mara kwa mara nyumbani kwetu mambo ya kutujazia choo mie siyataki. Kauli chafu kama hizi huyo sio mwanamke wa kuoa.
–
4. HAFANYI IBADA HATA KIDOGO
Mwanamke asiefanya ibada anapunguza hata baraka ndani ya nyumba na anatengeneza msingi mmbaya kwa watoto atakao zaa hafai.
–
5. MTOA SIRI ZA NDANI
Jambo dogo kasharusha Instagram au kawaeleza mashoga zake. Hana kaba hata kidogo muda wote kinywa chake kinamwaga radhi kwa kuanika siri za mumewe huyo usioe.
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT