Mwandishi wa Habari wa Ufaransa Frédéric Leclerc-Imhoff (32) ameuawa kwa kupigwa risasi nchini Ukraine.
–
Leclerc-Imhoff alikuwa akifanya kazi katika Shirika la habari la BFM TV na alikuwa nchini Ukraine kutangaza hali halisi ya vita ikiwemo uokoaji wa watu.
Kupitia mtandao wa Twitter Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameandika ya kuwa mwandishi huyo alikuwa ndani ya basi pamoja na raia wakijaribu kukimbia mabomu ya Urusi.
ADVERTISEMENT
–
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Catherine Colonna amesema kuwa ameshtushwa na habari hizo na anaomba uchunguzi wa wazi na wa kina kufanyika haraka iwezekanavyo.
ADVERTISEMENT