Mtangazaji wa Clouds Media, Mwemba Burton maarufu Mwijaku amekutwa na kesi ya kujibu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
–
Ni baada ya Serikali kufunga ushahidi wao wa mashahidi watano na vielelezo vinne walivyoviwasilisha wakati wa ushahidi.
–
Mwijaku anakabiliwa na shtaka moja la kusambaza picha za utupu kinyume cha sheria.
–
Anadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Septemba 17, 2019 na Oktoba 2019 katika jiji la Dar es salaam. Katika kipindi hicho, Mwijaku anadaiwa kuchapisha picha za ngono kupitia mtandao wa kijamii wa WhatsApp uliounganishwa katika kompyuta.
–
Mshtakiwa huyo anadaiwa kusambaza picha hizo huku akijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria. Kwa uamuzi wa jana, Mwijaku atatakiwa kujitetea dhidi ya shtaka linalomkabili.
–
Mwijaku ameieleza mahakama kuwa atajitetea kwa kiapo na kwamba anatarajia kuita mashahidi watatu kupangua shitaka linalomkabili. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 10, 2022 ambapo Mwijaku ataanza kujitetea.