Muigizaji staa Wema Sepetu hatimaye amemtolea uvivu shabiki ambae alimwambia kuwa amekonda sana hivi anakula kweli milo mitatu ndipo Wema alipomjibu kwa kumwambia aache kumfatilia kwani yeye anaupenda mwili wake na hata mpenzi wake anaupenda pia.
Akimjibu shabiki huyo,Wema aliandika hivi : “Ningekuwa tukunyema pia mngeniambia nipunguze milo…. Ebu niacheni na mpambane na mwili wangu huu… Mimi binafsi naupenda… Tukiachana na mimi binafsi, shem kama shem ndo haelewi kabisaaaaaa mambo ya mabonge…. wewe ni nani kuniamulia…??? Tulia na wewe unywe ukwaju na apple cider upunguze kilo kama rahisi… Tusiharibiane siku pulizzzzz….🤦🏼♀️🤦🏼♀️”