Netflix imesitisha mwendelezo wa filamu ya Pearl, iliyoandaliwa na Meghan Markle, katika harakati zake za kupunguza gharama.
–
Filamu hiyo ambayo ilitangazwa mwaka jana, ni moja ya miradi kadhaa iliyositishwa na gwiji wa kuonesha filamu.
–
Mwezi uliopita, Netflix ilibainisha kushuka kwa kasi ya waliojisajili na kutoa angalizo kuwa mamilioni zaidi ya watu wako tayari kuacha kutumia huduma hiyo.
–
Hiyo ilipunguza zaidi ya $50bn kutoka kwa thamani ya soko ya kampuni hiyo huku wataalam wakionya kuwa inakabiliwa na shida kurejea kwenye soko.
–
Archewell Productions, kampuni iliyoundwa na Duke na Duchess ya Sussex, ilitangaza mwaka jana kwamba Meghan atakuwa mtayarishaji mkuu wa Pearl.
–
Mfululizo wa filamu hiyo ulipangwa kuzingatia matukio ya msichana wa miaka 12, ambaye ameongozwa na wanawake wenye ushawishi kutoka kwa historia.
Credit – BBC Swahili.