Kocha wa Simba, Pablo Franco, raia wa Hispania, amefichua kuwa kilichobaki kwa sasa ni kuendelea kuwaombea wapinzani wao Yanga waendelee kupata matokeo mabaya huku wao wakiendelea kufanya vizuri kwa malengo ya kutwaa ubingwa wa msimu huu.
–
Pablo ametoa kauli hiyo kufuatia Simba kufikisha pointi 49 ikiwa ni tofauti ya pointi nane na vinara wa Ligi Kuu Bara, Yanga, wanaoongoza kwa pointi 57 baada ya suluhu tatu mfululizo.
–
Akizungumza na Championi Ijumaa, Pablo alisema wanachokifanya kwa sasa ni kuhakikisha wanapata matokeo ya ushindi katika kila mchezo huku wakiendelea kuwaombea mabaya wapinzani wao katika michezo iliyobakia kabla ya kumaliza ligi.
–
“Tumebakisha pointi nane ili kuweza kuwafikia, bado ni pointi nyingi kulingana na mechi ambazo zimabakia kabla ya kumaliza ligi, japo kwa sasa tukiwa sawa kwa idadi ya mechi ambazo tumecheza lakini kitu kikubwa tunachokiangalia ni kuhakikisha tunashinda kila mchezo ambao upo mbele yetu.
Credit – Championi