KOCHA wa Simba, Pablo Franco hajaridhishwa na kiwango kilichoonyeshwa na timu yake katika mechi yao waliyoshikiliwa kwa sare ya 1-1 dhidi ya Geita Gold kwenye Uwanja wa CCM Kirumba na kuwaweka mahasimu wao, Yanga jirani zaidi na kombe, akisema anataka kikao kizito na wachezaji wake.
–
Akizungumza na Mwanaspoti Pablo alisema sare ya hiyo imemnyima raha kwa sababu wachezaji wake hawakupambana kiasi cha kutosha.
–
Pablo alisema kuwa timu yake haikuonyesha ubora mkubwa kwa heshima ya jina la Simba na kwamba anataka kufanya kikao na wachezaji wake kujua shida ipo wapi kabla ya kukutana na watani wao Yanga kwenye mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Mei 28, hapohapo Uwanja wa CCM Kirumba.
–
“Hatukuwa na mchezo bora sana, hatukucheza soka letu ambalo tunajivunia siku zote, tulikuwa katika ubora mdogo, hili sio soka ambalo Simba inatakiwa kucheza,” alisema Pablo