ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Saturday, July 2, 2022
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result

“PANYA ROAD” KAENI CHONJO SERIKALI IPO KAZINI

Ally Hamis Zingizi by Ally Hamis Zingizi
May 19, 2022
in HABARI
0
“PANYA ROAD” KAENI CHONJO SERIKALI IPO KAZINI
0
SHARES
46
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

RelatedPosts

WATU WATANO WAFARIKI DUNIA KWA AJALI

WATU WATANO WAFARIKI DUNIA KWA AJALI

Jul 2, 2022

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMAMOSI JULAI 2, 2022

Jul 2, 2022

Benki ya NBC yawapiga jeki wakulima kwa mikopo ya trekta.

Jul 2, 2022
Load More

Kutoka Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Emmanuel Ludigija, Waziri wa Mambo ya Ndani Hamadi Masauni, Waziri Dkt. Dorothy Gwajima na Kamanda wa Polisi kanda Maalum ya Dar es Salaam Jumanne Muliro.wakati wa Ziara hiyo.

Baadhi ya wananchi wa Kata ya Chanika wakiwasiliza Mawaziri hao hawapo pichani kwa Nyakati tofauti, wakati wa Ziara ya Mawaziri Dkt. Dorothy Gwajima na Ahmad Masauni.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maaalum Dkt Dorothy Gwajima wakibadilishana Mawili matatu na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Hamadi Masauni, walipofanya Ziara kwenye Mkoa huo wa Dar es Salaam kufuatilia mwenendo wa suala la Panya road na hatua zilizo chukuliwa na Mamlaka za eneo hilo.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maaalum Dkt Dorothy Gwajima akiongea na wananchi wa Kata ya Chanika jijini Dar es Salaam.

***************

Na WMJJWM, DSM

Mawaziri Dkt. Dorothy Gwajima wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum na Hamadi Masauni wa Mambo ya Ndani ya Nchi, wameuambia umma kuwa, vijana wadogo wanaovamia watu na kuwakata kwa silaha zenye ncha kali kisha kuwa pora hawana uwezo wa kushindana na serikali iwapo wananchi watakuwa bega kwa bega katika kutoa taarifa za Uhalifu na viashiria kwa mamlaka za Serikali.

Wakizungumza hapo jana, Mei 18, 2022, Jijini Dar es Salaam kwenye kata za Chanika, Zingiziwa na Buza jijini humo wamesema, uwepo wa Mshikamano wa wanajamii na Serikali ndio suluhu ya kutokomeza vikundi hivyo vya vijana wanakadiriwa kuwa na miaka kati 16 hadi 20 kiasi.

Akizungumza kwenye Mkutano wa Hadhara, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima, alisema kumomonyoka kwa maadili katika makuzi na malezi ndio chanzo kikuu cha uzalishaji wa Kundi hilo.

“Mpaka mtoto anakuwa hivyo, sio suala la usiku mmoja, unakuta anaanza kidogo kidogo na ninyi wazazi kwakuwa hamtengi muda wakuzungumza naye na kujua mienendo yake, anazidi kukuwa na tabia hiyo hadi anafikia hatua sasa yakujiunga kwenye makundi ya kihalifu kama hilo la Panya Road” alisema Dkt. Gwajima

Waziri Gwajima, ameonya baadhi ya wanajamii kuacha kumuangalia mtoto kwa niwa mtu mwingine na badala yake watoto wote wahesabike kuwa wanajamii, kwani katika malezi ya sasa, baadhi ya wazazi hupandwa na hasira mwanae anapo adhibiwa au kuonywa na mzazi mwingine hali inayo nyong’onyeza jitihada za malezi na makuzi.

“Yapata juma moja nilikuwa eneo la Mbezi Luis, wazazi waliweka bayana haya mambo, wakisema, malezi ya zamani yalishirikisha jamii nzima, lakini kwa nyakati za sasa, wazazi wengi huweza kukufokea pale unapojaribu kumuongoza mwanane kwenye maadili mema, hii sio sawa kwani kufanya hivyo, huyo huyo mwanao Pamoja na wewe kujenga Gorofa kutokana na kutokuwa na malezi bora Mwanao mwenyewe anaweza kukuchinja kwenye nyumba yako. Alisisitiza Dkt. Gwajima.

Naye Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Hamadi Masaun, akiongea kwenye Mkutano huo ambao pia ulishirikisha Viongozi wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, alisema amefarijika kusikia tayari vijana zaidi ya 61 wakiwa wanashikiliwa na jeshi la Polisi kutokana na Ushirikiano ulioneshwa na Jamii.

“Mwanzoni nilipokuja hapa kila mmoja wetu alikuwa na sura ya simanzi kutokana na hofu na woga ulikuwa umetanda, lakini leo mmeniambia tayari wapo ambao wanashikiliwa na vyombo vya dola, lakini wengine tayari wamefikishwa Mahakamani kwa ajili yakukabiliana na kesi zao, niwapongeze sana kwa hili” alisema Masauni.

Naye Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, alisema, kama Jeshi la Polisi kwenye Kanda hiyo wataendelea kufanya kazi kwa mujibu wa viapo vyao na hawata muonea muhali mtu yeyote ambaye atathubutu kucheza na Amani ya Mtanzania yeyote kwenye kanda hiyo.

“Tumefanya kazi kwa ukaribu sana na Polisi Jamii, hawa wamekuwa msaada mkubwa na kutuwezesha kuwapata baadhi ya wahalifu hao katika maeneo ya Chanika, Kunduchi Mtongani na Nyatira, ambapo baadhi ya watu waliokamatwa walikutwa na TV, Simu na vitu vingine vilivyo porwa kwenye matukio hayo.” Alisema Kamanda Muliro.

Nao wananchi wa Maeneo ya Chanika na Kata ya Buza hawakusita kuonesha furaha yao baada yakuwaona Mawaziri hao huku wakiwasifu na kumshukuru Waziri Gwajima kwa darasa la kamati za MTAKUWWA na majukumu yake.

Mawaziri Dkt. Gwajima na Masauni, kwa Pamoja na Kamanda wa Polisi kanda Maalum ya Dar es Salaam, walifanya ziara kwenye Kata za Chanika, na Buza na kuongea na wahanga wa matukio ya Panya Road yaliyokithiri kwenye jiji hilo ndani ya majuma mawili yaliyopita.

ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT

Related

ADVERTISEMENT
Ally Hamis Zingizi

Ally Hamis Zingizi

Related Posts

WATU WATANO WAFARIKI DUNIA KWA AJALI
HABARI

WATU WATANO WAFARIKI DUNIA KWA AJALI

by Shabani Rapwi
Jul 2, 2022
NEYMAR KUONDOKA PSG
HABARI

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMAMOSI JULAI 2, 2022

by Shabani Rapwi
Jul 2, 2022
Benki ya NBC yawapiga jeki wakulima kwa mikopo ya trekta.
BIASHARA

Benki ya NBC yawapiga jeki wakulima kwa mikopo ya trekta.

by I am Krantz
Jul 2, 2022
AFARIKI DUNIA BAADA YA KUNASA KWENYE NYAYA ZA UMEME
HABARI

AFARIKI DUNIA BAADA YA KUNASA KWENYE NYAYA ZA UMEME

by Shabani Rapwi
Jul 1, 2022
MTUMISHI WA TANESCO AKUTWA GUEST AMEFARIKI
HABARI

MTUMISHI WA TANESCO AKUTWA GUEST AMEFARIKI

by Shabani Rapwi
Jul 1, 2022
SIKUKUU YA EID EL-ADH’HAA JULAI 10, 2022
HABARI

SIKUKUU YA EID EL-ADH’HAA JULAI 10, 2022

by Shabani Rapwi
Jul 1, 2022

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
May 2022
M T W T F S S
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031  
« Apr   Jun »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In