Kocha wa Manchester City raia wa Hispania, Pep Guardiola ametupa dongo kwa klabu ya Liverpool kwa kudai klabu hiyo haina historia Ligi Kuu ya Uingereza.
–
Guardiola amedai Liverpool haina historia Ligi Kuu ya Uingereza kwasababu imechukua ubingwa wa Ligi hiyo mara moja baada ya kipindi cha miaka 30, Sambamba na kauli hiyo Guardiola ameisifia klabu hiyo kwa kuwa na mafanikio mazuri kwenye mashindano ya UEFA.
–
Manchester City imejikita kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu nchini Uingereza ikiwa na jumla ya alama 86 ikifuatiwa na Liverpool yenye alama 83 zote zikiwa zimecheza michezo 35.