Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharib Unguja limethibitisha kutokea kwa Ajali ya gari ambayo imesabibisha vifo vya watu wawili na Majeruhi watatu.
–
Akitoa taarifa ya awali ya Ajali hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharib Unguja Kamishna Msaidizi wa Polisi Abdalla Hussein Mussa amesema ajali hiyo imetokea Mei 23, 2022 majira ya asubuhi ambapo ajali hiyo iliyohusisha Gari aina ya Fuso yenye namba za usajili Z686 FV ambapo gari hiyo iliyokua ikitokea Kilamani Juu na kushukia Chini iliacha njia na kugonga Duka na gari.
–
Amesema waliofariki Dunia ni Asha Said Ali na Fatma Abeid Salum ambao walikua wakipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mnazi Mmoja Mjini Unguja