Ameandika Romantix Aloyce
–
“Mashabiki wa Professor Jay tunataka Taarifa kuhusu Msanii wetu. Ni muda mrefu sasa tangu tuambiwe amelazwa ICU pale Muhimbili, Familia ilihitaji Michango tukachanga hamasa ilikuwa kubwa sana.
–
Wa kuchanga tukachanga wa kumuombea wakamuombea lakini Ghafla imekuwa kimyaaa, hatujui Maendeleo ya Mgonjwa!!
–
Mashabiki zake tunataka kujua Prof Jay yuko wapi?? Yupo Hospitalini au alirudi Nyumbani? Na kama yupo Hospitalini anaendeleaje? Tunataka kujua Prof Jay yupo Hai au laah!. Naamini Familia itajitokeza kujibu maswali ya Watanzania sio kujibu tu watuonyeshe kabisa alipo Prof Jay.” Romantix Aloyce