Rais wa nchi za falme za kiarabu UAE Sheikh Khalifa bin Zayed Al Nahyan amefariki dunia leo akiwa na umri wa miaka 73.
–
Sheikh Khalifa aliteuliwa kuwa Rais wa pili wa UAE mnamo mwaka 2004 akimrithi baba yake Sheikh Zayed Al Nahyan.
–
Kipindi rasmi cha maombolezo kimeanza leo huko UAE na bendera zitapepea nusu mlingoti kwa siku 40.