Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan leo ameshinda tuzo mahiri ya Babacar Ndiaye Kwa mwaka 2022 katika mkutano mkuu wa Benki ya maendeleo Africa AFDB nchini Ghana.
–
Rais Samia ametunukiwa tuzo hiyo kutokana na usimamizi mzuri wa ujenzi wa miundombinu ya usafirishaji yaani barabara na reli.
–
Kamati ya tuzo imetoa pongezi Kwa Rais Samia na watanzania kwa mafanikio hayo, huku ikisisitiza wakuu wa nchi za Afrika kuongeza juhudi katika usimamizi na ujenzi wa miundombinu ya usafiri na usafirishaji.