Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suuhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kufuatia kifo cha aliyekuwa rais wa falme hizo Khalifa Bin Zayed Al Nahyan.
Rais Samia amendika ujumbe kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram uliosomeka:
“Ni kwa masikitiko makubwa tumepokea taarifa za kifo cha Sheikh Khalifa bin Zayed Al Nahyan, Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu na kiongozi wa Abu Dhabi, Sheikh Mohamed Bin Zayed, Familia ya kifalme na watu wa Umoja wa Falme za Kiarabu pokeeni salamu zetu za rambirambi.
Alikuwa kiongozi mzuri!”
Taarifa za kifo cha Bin Zayed zimetangazwa jana ambapo chanzo cha kifo chake ni maradhi ya muda mrefu ya kupooza aliyoyapata tangu mwaka 2014 yaliyomfanya awe mbali na macho ya watu, amefariki akiwa na umri wa miaka 73.