Aliyekuwa Meneja wa muda wa Manchester United, Ralf Rangnick ametangaza kuwa hatasalia klabuni hapo katika kitengo cha ushauri kutokana na uhitaji wa majukumu yake mapya ya kukinoa kikosi cha timu ya Taifa Austria.
–
Awali Mjerumani huyo alikubali kukinoa kikosi cha timu ya timu ya Taifa Austria huku akisalia kama mshauri wa klabu hiyo lakini sasa mambo yamebadilika.
–
Man United imesema: “Kwa makubaliano ya pamoja, Ralf atajikita zaidi na majukumu yake mapya ya timu ya Taifa Austria na hivyo hatachukua jukumu la kuwa mshauri Old Trafford”