Muimbaji na rapa maarufu nchini India Sidhu Moose Wala (28) ameuawa kwa kupigwa risasi.
–
Vyombo vya habari vya India vimeripoti kuwa Msanii huyo aliyekuwa na kipaji kikubwa kilichomletea umaarufu Kimataifa ameuawa katika wilaya ya Mansa huko Punjab.
ADVERTISEMENT
–
Mauaji hayo yamekuja siku moja baada ya serikali ya Punjab kumuondolea ulinzi yeye pamoja na watu wengine 429 kama sehemu ya mpango wa kuondoa utamaduni wa kuwaona watu kadhaa kuwa wana umuhimu mkubwa sana “VIP”.
–
ADVERTISEMENT
Sidhu alikuwa Mgombea katika uchaguzi wa mwaka huu wa Punjab kwa tiketi ya chama cha Congress.