Klabu ya Simba imefikia makubaliano ya pande zote mbili ya kuvunja mkataba na Kocha Mkuu wa timu hiyo Pablo Franco Martin.
–
Katika kipindi chake Kocha Pablo ameiwezesha timu ya Simba kutwaa ubingwa wa kombe Ia Mapinduzi na kufika robo fainali ya kombe Ia Shirikisho Barani Afrika.
–
Katika kipindi chote cha kumalizia msimu kikosi lhicho cha Wekundu wa Msimbazi kitakua chini ya Kocha Msaidizi Selemani Matola.
ADVERTISEMENT
–
Vilevile klabu ya Simba imefikia makubaliano ya pande zote mbili ya kuvunja mkataba na kocha wa viungo Daniel De Castro Reyes.
ADVERTISEMENT