MSANII wa muziki wa Bongofleva na boss wa lebo ya Next Level Music, Raymond Shaban Mwakyusa Maarufu Rayvanny ameweka rekodi kwa kufikisha streams milioni 100 kupitia music platform ya Boomplay.
–
Rayvanny ambaye pia ni member wa lebo kubwa barani Africa WCB Wasafi, amekuwa msanii wa kwanza nchini kufikisha streams milioni 100 kupitia platform hiyo, akiwakalisha wasanii kibao akiwemo Boss wake Diamond Platnumz.
–
Kwa hatua hii, @Rayvanny anajiunga na wasanii wengine wakubwa Africa kama vile Burna Boy, Olamide, Fireboy DML kwenye Golden Club ya Boomplay.
Kupitia platform ya Boomplay, Rayvanny ndiye msanii wa Kitanzania anayefuatiliwa zaidi akiwa na jumla ya wafuasi zaidi ya 150k, huku EP yake ya Flowers II ikiwa ndio kazi yake iliyosikilizwa zaidi Boomplay ikiwa na zaidi ya streams 30m. Albamu yake ya Sound from Africa yenye zaidi ya wasikilizaji milioni 22.9 ni albamu ya nne ya Tanzania ambayo imesikilizwa zaidi baada ya ‘Definition of Love’ ya Mbosso, Album ya Alikiba ya ‘Only One King’, na Albamu ya Harmonize ‘High School’.