Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla ametangaza kuanza kwa maalum usiku wa leo ya kupambana na kundi la vijana linalofanya uvamizi na kuiba majumbani maarufu kama ‘Panya Road’ katika mkoa wa Dar es Salaam.
–
RC Makalla ameyasema hayo katika kikao na Makamanda wa Polisi wa mkoa pamoja na wakuu wa vituo vya polisi ili kujadili kadhia hiyo iliyoanza katika kipindi cha hivi karibuni katika baadhi ya maeneo ndani ya jiji hilo.
–
“Hatutoruhusu Panya Road watie hofu jamii, ni wakati wakuwaonya kuanzia leo baada ya tamko langu, usiku wa leo na kuendelea hakuna panya road atasalimika katika mkoa wa Dar es Salaam, operesheni hii inaenda kuua uti wa mgongo wa mtandao mzima wa Panya Road katika mkoa wa Dar es Salaam, wakachague kazi zingine za kufanya,” amesema RC Makalla.