Waziri wa Maliasili na Utalii balozi, Dkt. Pindi Chana ameridhishwa na kazi nzuri zinazofanywa na chuo hicho cha utalii Tanzania, huku akieleza namna Filamu ya Royal Tour ilivyoanza kutoa matokeo Chanya.
–
Wazir Dkt Chana amesema hayo baada ya kutembelea chuo hicho kwa lengo la kujionea shuhuli mbalimbali zinazofanyika chuoni hapo ambapo amewataka kuanzisha taala maalumu ya kuwapokea watalii.
–
Aidha amempongeza na kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa uzinduzi wa filam ya Royal Tour ambapo amesema filamu hiyo inakwenda kufungua milango ya utalii na takwim zinaonyesha tangu uzinduzi wa filamu hiyo watalii wameongezeka nchini.